
UTANGULIZI
Kutokana na ushauri hai wa mheshimiwa-sasa mstaafu-Askofu Mkuu wa Trani, Askofu Yosefu Carata, nilisukumwa kuweka kwa maandishi, ushuhuda juu ya Luisa Piccaretta, uliokusanywa kwa sauti hai na ndugu zangu na watu wengine waliomfahamu binafsi, mtumishi huyo wa Mungu. Katika baadhi ya matukio, nilihusika mimi mwenyewe, moja kwa moja.
Katika utoto wangu, nimekutana daima ana kwa ana, na mtumshi wa Mungu. Mikutano hiyo, ilirahisishwa na shangazi yangu, Rosaria Bucci ambaye, kwa karibia miaka arobaini, alisaidia, usiku na mchana, Mtumishi huyo wa Mungu. Watu hao wawili, walifanya kazi pamoja kwenye nakshi wakichora ya bahati nasibu na kupata riziki yao.
Jamaa zangu waliunganishwa na vifungo vingi kwenye familia ya Piccarreta. Dada zangu, Isa, Maria na Gemma, walikwenda mara kwa mara bila kuchoka kwao Luisa, pia kwa ajili ya kujifunza nakshi ya bahati nasibu. Gemma mdogo zaidi alipendwa zaidi na Luisa, ambaye ndiye alipendekeza aitwe kwa jina hilo wakati wa kuzaliwa kwake. Dada yake na Luisa, Angelina, alikuwa ni mama wa ubatizo na kipaimara wa dada zangu. Tulipendana naye kiasi kwamba, katika familia yetu, wote walimwita” shangazi Angelina.” Na Luisa, mtu alizungumza bila kuogopa. Ninakumbuka, kwamba mama alienda nyumbani kwa Luisa, na kukaa naye kwa muda mrefu. Hakuna anayejua mazungumzo yao yalikuwa juu ya nini. Ninaamini kwamba, Luisa alikuwa amemtabiria kifo chake kabla ya wakati wake. Ninafikiri hivyo, kutokana na jambo la kwamba, mama, mara mojamoja alikuwa anazungumza juu ya kifo, na alitufanya tuelewe kwamba asingeishi miaka mingi. Alifariki akiwa na umri wa miaka hamsini na moja, miaka mitatu baada ya kuondoka (kifo) kwa Luisa. Wakati wa kuondoka kwake, alikuwa amevaa shati la Mtumishi wa Mungu. Mimi mwenyewe nilipata kutoka kwa mtumishi wa Mungu sanamu ya watakatifu na tuvinyago. Licha ya kuzoeana kwetu, mbele ya Luisa nilikuwa ninakaa kimya, nikiwa kama nimenuiziwa kwa mvuto kutoka kwake. Nilikusanya mambo mengi na taarifa, yaliyoandikwa lakini siwezi kupanga yote hayo, kwa ajili ya kuyachapisha, jambo ambalo lingehitaji kazi nyingi na muda wa kutosha, ambao sikuwa nao au haukuniruhusu. Nimepaswa kuchagua, na kuchapisha yale ambayo niliamini kwamba, Ya nafaa na kupendeza zaidi.
Kwa jambo hilo, sipendi kusema kuwa matukio mengine yaliyosajiliwa, hayastahili kufahimika. Mimi ninaamini kabisa kwamba, tukio, lolote lile linalomhusu Piccarreta, linafaa kwa kuchora picha yake.
Luisa Piccaretta
Kwa wakati wake: Ninaahidi kuendeleza kazi hii ya kupanga na kufanya utafiti wa kumbukumbu na kuwapa wachapaji, mambo kamili ya mtumishi wa Mungu (historia). Kazi iliyoanzishwa kwa nyakati tofauti, na ambayo ninatumaini kumaliza mapema iwezekanavyo.
SURA YA KWANZA
VIDOKEZO VYA KIHISTORIA VYA MAISHA YA LUISA
Mtumishi wa Mungu, Luisa Piccarreta alizaliwa Corato, katika Jimbo la Bari, tarehe 23 Aprili mwaka 1865, na alifia kule akifikiriwa kuwa mtakatifu, mwaka 1947.
Luisa alikuwa na bahati ya kuzaliwa katika moja ya familia za kipatriaki, ambazo hata katika mazingira yetu ya Jimbo la Puglia, zinapenda kuishi mahali wazi, mashambani. Wazazi wake, Vito Nikola na Rosa Tarantino, walikuwa na watoto watano, yaani Maria, Racheli, Filomena, Luisa na Angela. Maria, Racheli na Filomena waliolewa. Angela, aliyejulikana kwa kawaida kama Angelina, alibaki bila kuolewa, karibu na dada yake Luisa mpaka kufa.
Luisa alizaliwa siku ya Jumapili ya pili baada ya Pasaka, inayojulikana kama “Dominica in Albis,” na alibatizwa siku hiyo hiyo. Baba yake, saa chache baada ya kuzaliwa kwa Luisa alimfunga ndani ya blanketi na kumpeleka parokiani, ambako alibatizwa. Nicola Piccarreta alikuwa ni mtunzaji wa shamba moja, mali ya familia ya Mastrorilli, iliyokuwa katikati mwa Murge, kwenye sehemu inayoitwa Torre Disperata, Kilomita 27 kutoka Corato. Mtu anayefahamu sehemu hizi, anaweza kusifia hali kuu ya utulivu, ukimya inayotawala kule, ikiwa imezama kabisa kati ya vilima huru visivyo na jani wala mti wowote juu yao, na vyenye kujaa mawe. Katika shamba hili, Luisa alikaa kwa muda wa miaka mingi ya utoto wake na ujana wake. Mbele ya msururu wa majengo makubwa.
LUISA PICCARRETA
Kuna bado mti wa fahari na wa mviringo wa aina ya mforsadi, wenye shimo kubwa katika shina lake, ambamo Luisa katika utoto wake, alikuwa akienda kujificha na kusali, mbali na macho yasiyokuwa na busara. Ni mahali hapa pa upweke na uhuru, ambapo, kwa Luisa, palianzia tukio la Kimungu litakaloongoza nyayo zake za mateso na za utakatifu. Hasa, ilikuwa ni mahali hapo ambapo alipata mateso yasiyoweza kuelezeka ya kushambuliwa na mwovu ambaye mara moja moja, alimtesa vibaya sana, hata kimwili. Luisa, ili awe huru mbali na mateso ya aina hii, bila kukoma, alikimbilia kusali, akimgeukia kwa namna ya pekee, Bikira Mtakatifu sana, ambaye alimfariji na uwepo wake.
Kudra ya Mungu ilimwongoza msichana huyu, kwenye njia zisizoeleweka kiasi kwamba, hakuweza kujua furaha nyingine tofauti kuliko ile ya kwamba, Mungu ndiye neema au UZIMA WAKE. Hasa, siku moja Bwana alimwambia: “Mimi nilizunguka tena na tena duniani, nikangaalia kila kiumbe, kimoja kimoja, ili nione ni kipi kilikuwa kidogo zaid kuliko vyote. Kati ya vyote hivyo, nilipata wewe, kadogo zaidi kuliko vyote. Kati ya vyote hivyo, nilikupata wewe kadogo zaidi kuliko vyote. Udogo wako ulinifurahisha na nikakuchagua; nilikukabidhi kwa malaika wangu, hadi wakulinde salama, si kwa ajili ya kukufanya mkuu, ila watunze udogo wako na sasa ninataka kuanza kazi kubwa ya kukamilisha utashi au mapenzi yangu. Wala si kwa hilo, kwamba utajisikia mkuu zaidi, hasa utashi au mapenzi yangu yatakufanya uwe mdogo zaidi, na utaendelea kuwa binti mdogo zaidi, wa Utashi wa Mungu. ” (cfr.Volume- Juzuu 12, March 1921
Akiwa na umri wa miaka tisa, kwa mara ya kwanza, Luisa alipokea Yesu wa Ekaristi na Kipamara, na tangu hapo, akajifunza kudumu katika sala, kwa saa nyingi mbele ya Sakramenti Takatifu. Alipotimiza miaka kumi na mmoja, alipenda kujiandikisha kwenye Shirika la Mabinti wa Maria lililokuwa linastawi sana wakati huo katika Kanisa la Mtakatifu Yosefu. Alipofikisha umri wa miaka kumi na minane, Luisa alikuwa mwanashirika wa daraja la Tatu la Wadominikani, na kuitwa jina la Sista Magdalena. Alikuwa kati ya watu wa kwanza, kujiandikisha kwanye Daraja la Tatu, ambalo kwalo, Paroko wake ndiye alikuwa msimamizi. Ibada ya Luisa kwa Mama wa Mungu, itaongeza ndani mwake hali ya kiroho ya kina kingi kwa Maria, utangulizi wa kile ambacho siku moja atapaswa kuandika juu ya Mama yetu.
Sauti ya Yesu ilikuwa inamwongoza Luisa katika kunasua nafsi yake mwenyewe, kutoka kwa kila kitu na kila mtu. Akikaribia umri wa miaka kumi na minane, kutoka kwenye kibaraza cha nyumbani kwao, katika barabara ya Nazario Sauro, Luisa alipata maono ya Yesu akiwa ametundikwa juu ya Msalaba, ambaye alipoinua macho juu na kumwangalia, alitamka maneno haya: “ Roho, nisaidie!” Ilikuwa ni kutoka wakati huo, tamaa isiyoweza kuridhishwa, ilishuka na kuingia ndani ya Luisa, tamaa ya kupenda kuteswa kwa ajili ya Yesu,na kwa ajili ya wokovu wa roho za watu. Hivyo, mateso hayo ya kimwili yalianza, ambayo yakiwa yameungana na yale ya kiroho na kimaadili, yalifikia kwenye ushujaa.
Familia ilibadilishana au kugawana,hali hizi kwa ajili ya ugonjwa, na kutafuta msaada wa kisayansi. Lakini waganga wote walioitwa, walizidi kushangaa mbele ya kesi moja ya matibabu, isiyo ya kawaida na ya pekee kabisa. Mwili wa Luisa, ulikuwa unakuwa mweupe kama maiti, hata kama kulikuwa na dalili za uzima au maisha, na hakukuwa na tiba zozote zilizoweza kumpa nafuu kutoka katika mateso haya yasiyweza kuelezeka.
Busara au maarifa yote ya kisayansi yalipokuwa yametumika yote, watu walikimbilia kwenye tumaini la mwisho; yaani, mapadre. Padre mmoja, alipoitwa kandokando ya kitandana chake, Padre Cosma Loiodice wa Shirika la Mt. Augustine, aliyekuwa kwenye familia hiyo, kwa mshangao wa kila mtu aliyekuwa pale, alipiga ishara ya msalaba, ambayo Padre aliifanya kwenye mwili huo maskini, kwa ajili ya kumrudisha mara moja kwenye hali yake thabiti, ya kawaida na ya nguvu zake. Baada ya Padre Loiodice kuondoka na kuelekea kwenye konventi, mapadre wengine wanajimbo waliitwa, ambao kwa ishara ya msalaba, walimrudisha Luisa katika hali yake ya kawaida. Yeye Luisa alikuwa anaamini kwamba, mapadre wote ni watakatifu, lakini siku moja Bwana alimwambia hivi: “Si kwa sababu wote ni watakatifu, walau wangekuwa hivyo, ila tu kwa sababu wao ni mwendelezo wa Upadre wangu duniani, wewe daima unapaswa kuwa chini ya mamlaka yao, usipingane nao hata kidogo, wema na wabaya wanaoweza kuwepo.”(cfr. Juzuu I).
Luisa daima atakuwa chini ya mamlaka ya kipadre, maisha yake yote. Hilo litakuwa ni moja ya mambo ambayo yatafanya ateseke zaidi. Haya ya kila siku ya mamlaka ya kipadre, au kurudi kwenye shughuli za mwanzoni, mashinikizo na mateso ya kudhalilisha sana, aliyavumilia, hasa upande wa mapadre ambao walimwona kama msichana mtukufu, mwehu, mtu aliyependa kuonekana na wengine. Wakati fulani walimwacha katika hali hiyo kwa siku ishirini au zaidi. Luisa baada ya kukubali kuwa kafara, aliishi hali moja peke yake sana; yaani, kila asubuhi alijikuta amekakamaa, bila kujitikisa, amejikunyata juu ya kitanda chake, wala hakuna mtu yeyote aliyeweza kumnyoosha, kuinua mikono yake, kuinua kichwa chake au miguu yake. Kama tunavyojua uwezo wa padre ulikuwa wa lazima, padre ambaye kwa kumbariki, kwa ishara ya msalaba, aliondoa ukakamavu huo, kama wa mwili wa mtu aliyekufa, na kumfanya arudi kwenye kazi zake za kawaida za kuchezesha bahati nasibu.
Kesi ya pekee; yaani, waungamishi wake, hawakuwa hata siku moja wakurugenzi wake wa kiroho, kazi ambayo Bwana wetu alipenda kujibakizia yeye mwenyewe. Yesu alimfanya asikie moja, kwa moja sauti yake ikimfundisha, kumkanya, kama ilibidi, na polepole alimpeleka hadi kwenye vilele vya juu sana vya ukamilifu. Luisa, akijua, alifundishwa na mwenye kuwa tayari, kwa miaka mingi au mirefu, kupokea zawadi ya Utashi wa Mungu.
Askofu Mkuu wa wakati huo, Yosefu Bianchi Dottula, tarehe 22 Desemba 1848 hadi Septemba tarehe 22, mwaka 1892, baada ya kufahamu yale yaliyokuwa yanatokea, katika sehemu ya Corato, baada ya kusikiliza mawazo ya mapadre wengine, alipenda kuweka chini ya mamlaka yake na uwajibikaji wake, kesi hiyo, na baada ya kutafakari kikamilifu, aliamini kwamba, ilikuwa ni wakati mwafaka, kumpa mamlaka maalum kama muungamishi wa pekee, padre aliyeitwa, Don Michele de Benedicts, mfano mzuri sana wa Padre, ambaye kwake, Luisa alifungua kidogokidogo roho yake. Don Michele, mwangalifu, mwenye maisha matakatifu, aliweka mipaka kwenye mateso yake, na yeye (Luisa) hakupaswa kufanya kitu chochote, bila Don Michele kukubali. Hasa alikuwa ni Don Michele aliyemwamuru (Luisa) ale, angalau, mara moja kwa siku, hata kama mara baada ya kula alitapika. Luisa alipaswa kuishi kwa utashi au mapenzi ya Mungu tu. Ilikuwa ni chini ya padre huyo kwamba, aliruhusiwa kubaki daima kitandani, akiwa kafara wa malipizi.
Ilikuwa ni mwaka 1888, Luisa alibaki amepigiliwa misumari kwenye kitanda chake na maumivu, akiwa daima ameketi kwa kipindi cha miaka mingine hamsini na tisa, mpaka kifo chake. Ni jambo la kukumbukwa kwamba, hadi wakati huu, Luisa, licha ya kukubali hali ya kuwa kafara, aliendelea kubaki kitandani, daima akibadilika mara kwa mara, kwa sababu utii haukumruhusu hata siku moja, kubaki kitandani kwa namna ile ile. Lakini, tangu mwanzoni mwa mwaka 1889 hadi tarehe 13 mwezi Mei 1906, alimtuma kama muungamishi mpya, Don Gennaro Di Gennaro, aliyefanya kazi hiyo kwa muda wa miaka ishirini. Muungamishi huyu mpya, akiona maajabu ambayo Bwana aliyafanya katika roho huyu, alimwamuru bila kusita, Luisa kuandika yote yale ambayo kwa Neema ya Mungu, aliyafanya ndani mwake. Hoja zote zilizotolewa na Mtumishi wa Bwana, hazikufaa kitu kwa kuwa mbadala wa kutii wa muungamishi wake, yaani, hata matayarisho yake ya kiuandishi ya nadra sana, hayakuweza kumwondoa kwa utii.
Don Gennaro Di Gennaro alibaki baridi bila kujitikisa, licha ya kujua kwamba, maskini huyo, alimaliza shule ya msingi tu. Hivyo ndivyo ulivyokuwa mwanzo, tarehe 28 mwezi Februari mwaka 1889, wakutungwa kwa kitabu chake cha kumbukumbu, chenye juzuu kubwa zipatazo thelathini na sita! Sura ya mwisho ilimalizika tarehe 28 Desemba mwaka 1939, siku ambapo alikatazwa asiandike tena.
Muungamishi wake alipofariki, tarehe 10 Septemba, mwaka 1922, Don Francesco De Benedicts alichukua nafasi yake, ambaye alimsaidia Luiza kwa miaka minne tu, kwa sababu alifariki tarehe 30 mwezi Januari, mwaka 1926. Askofu Mkuu,Giuseppe. Leo, aliyekuwa Askofu tangu tarehe 17 Januari mwaka 1920, hadi tarehe 20 mwezi Januari mwaka 1939, alimtuma, kama muungamishi wa kawaida, padre mmoja kijana, Don Benedetto Calvi, ambaye alibaki karibu na Luisa, hadi kifo chake, akigawana mateso yote yale, na wasiwasi ambavyo vilimgonga Mtumishi wa Bwana, katika miaka ya mwisho ya maisha yake.
Mwanzoni mwa Karne, watu wetu walipata bahati ya kuona, Mwenyeheri Hanibal Maria Di Francia, ambaye alitaka kufungua nyumba moja ya wanawake ya Shirika lake, lililokuwa ndo linazaliwa Trani, akizunguka katika sehemu ya Puglia. Alimpomfahamu Luisa Piccarreta, alienda kumtembelea, na tangu wakati huo, roho hizi mbili kuu, zilifungwa pamoja kwa kutoweza kutenganishwa tena, kwa vyovyote vile. Hata mapadre wengine mashuhuri walienda kumwona Luisa mara kwa mara, kama kwa mfano, Padre Myesuiti Gennaro Braccali, Padre Eustachio Montemurno, na Don Fernando Cento, Mjumbe wa Papa na Kardinali wa Mama Mtakatifu wa Kanisa. Mwenyeheri Hannibal, alikuwa muungamishi wake asiye wa kawaida, na msahihihaji wa maandishi yake au vitabu vyake, ambavyo, kidogokidogo, vilichunguzwa mara kwa mara na kupitishwa au kukubaliwa, na mamlaka au viongozi wa Kanisa.
Karibia kwenye mwaka 1926, Mwenyeheri Hannibal alimwamuru Luisa aandike daftari moja la kumbukumbu za utoto na ujana wake. Mwenyeheri Hannibal alichapisha maandishi mbalimbali juu ya Luisa, ambayo kati yao, kilibaki kitabu maarufu kinachoitwa, SAA YA MATESO, ambacho kilichapishwa mara nyingi, hasa mara nne.
Tarehe 7 mwezi Octoba mwaka 1928, illikuwa imeisha kujengwa nyumba ya masista wa Shirika la Hamasa au Ari ya Kimungu katika sehemu ya Corato, kwa kuhamasisha hamu ya mwenyeheri mwenyewe Hannibal, Luisa alihamishwa na kupelekwa kwenye konventi hiyo. Mwenyeheri Hannibal alikuwa tayari amefariki, akisifiwa kama mtakatifu katika sehemu ya Messina.
Mwaka 1938 Luisa alipata pigo kubwa sana la dhoruba, yaani, alikataliwa hadharani na Roma, na vitabu vyake vikawekwa kwenye fahirisi, au ordha ya vitabu vilivyopigwa marufuku kusomwa. Kwenye kutangazwa kwa laana ya Ofisi Takatifu, Luisa, moja kwa moja, aliwekwa chini ya mamlaka ya Kanisa. Kutoka Roma, akiwa ametumwa na uongozi wa Kanisa, alijitokeza Padre mmoja, ambaye alimwomba Luisa maandishi yote, aliyoyandika kwa mkono wake. Kwa namna hiyo, maandishi au vitabu vyote vilifungiwa ndani ya siri za Ofisi Takatifu.
Tarehe 7 mwezi Octoba mwaka 1938, kwa amri ya wakuu, Luisa alipaswa kuacha konventi, na kutafuta makao mengine mapya. Baada ya kupita miaka yake tisa ya mwisho ya maisha yake, katika nyumba moja, kwenye barabara ya Magdalena, sehemu ambayo wazee wa Corato wanaifahamu vizuri, na ambako, tarehe 8 mwezi Machi mwaka 1947, waliona maiti yake ikitolewa. Maisha ya Luisa yalikuwa ya kiasi sana, yeye alikuwa na mali au vitu vichache au bila kitu chochote. Alikuwa anaishi katika nyumba ya kupanga, akisaidiwa kwa upendo na dada yake Angela, na wanawake wengine wacha Mungu. Kile kidogo alichokuwa nacho, hakikutosha hata kwa njiwa wa nyumbani. Kwa chakula chake, alikuwa anafanyakazi kwa bidii sana, kwenye bahati nasibu, akichukua kile tu kilichomtosha, kwa kumfunza dada yake, kwa kuwa yeye hakuhitaji, wala nguo au mavazi, wala viatu. Chakula chake kilikuwa ni kiasi kidogo ambacho alipewa na msaidizi wake Rosaria Bucci. Luisa alikuwa haagizi kitu, wala kutamani kitu, na alikuwa anarudisha au kutapika mara moja, kile alichomeza. Hali yake haikuwa ile ya mtu aliyekuwa kufani, lakini, hata hivyo, si kama ile ya mtu aliyekuwa na afya yake kamili. Hata hivyo, alikuwa hakai bure, nguvu zake ziliishia, au zilimalizwa, au na mateso ya kila siku, au katika kazi na maisha yake, kwa yule aliyeyafahamu kwa kina sana, yalifikiriwa kuwa ni muujiza wa daima. Cha kushangaza, kilikuwa ni yeye, kutong’ang’ania kwenye faida yoyote ambayo alipewa kwa sifa yoyote ile.
Hakukubali hata mara moja fedha, zilizotokana na kuchapishwa kwa vitabu vyake. Hivyo, siku moja alimjibu Hannibal aliyetaka kumpa fedha, kutokana na haki yake, kama mwandishi wa kitabu na kusema: “ Mimi sina haki yoyote, kwa sababu, kile kilichoandikwa mule, si changu.(cfr. “PREFAZIONE” to the book “Saa ya Mateso” Messina, 1926). Alikuwa anakataa kwa ukali na kurudisha fedha, ambayo, wakati mwingine, watu wacha Mungu walimtumia.
Makao ya Luisa yalikuwa yanafanana kama monasteri moja, hakuna mjuviaji yeyote aliyeingia kule. Luisa alikuwa amezungukwa na wanawake wachache, waliokuwa wanakuja kwenye mambo yaleyale ya ki-roho, alizungukwa pia na wasichana fulani, walioenda mara kwa mara nyumbani kwake, kwa ajili ya kujifunza kutarizi, kwenye mchezo wa bahati nasibu. Ilikuwa hasa, ni pale kwenye chumba cha karamu ya mwisho “cenacolo,” ambako ilitoka idadi kubwa ya miito ya watawa. Lakini, kazi yake ya malezi, haikuishia tu kwa wasichana vijana, wengi wa kiume walikuwa wanapelekwa naye kwenye taasisi kadhaa za kitawa na upadre.
Siku yake ilianza asubuhi, karibia saa kumi na moja, wakati padre alifika nyumbani, kwa ajili ya kumbariki na kusoma Misa Takatifu, iliyokuwa inaongozwa na muungamishi wake, au mwingine aliyetumwa kufanya vile, upendeleo uliochukuliwa kutoka kwa Leo XIII (wa kumi na tatu), na kuthibitishwa na Mtakatifu Pio X (wa kumi), mwaka 1907. Baada ya Misa Takatifu, Luisa alibaki akisali sala za shukrani, kwa karibia muda wa saa mbili. Kuelekea kwenye saa mbili, kazi yake ilianza, ambayo iliendelea hadi mchana; baada ya chakula cha kiasi cha mchana, Luisa alibaki peke yake chumbani mwake, akikazia mawazo yake mahali fulani. Adhuhuri, baada ya saa kadhaa za kazi, alisali Rosari. Jioni, kuelekea kwenye saa mbili, Luisa alianza kuandika kitabu chake cha kumbukumbuku; usiku wa manane alilala usingizi. Asubuhi alijikunyata kitandani, kichwa chake kikiwa kinaelekea au kuinamia upande wa kulia, na ilikuwa ni lazima kuita msaada wa mamlaka ya kipadre, ili kumwita tena kwenye kazi zake na kumketisha kwenye kitanda chake.
Luisa alifariki akiwa na umri wa miaka themanini na moja, miezi kumi na siku tisa, tarehe 4 mwezi wa Machi mwaka 1947, baada ya kuugua kwa muda wa siku kumi na tano; ugonjwa pekee ambo ulihakikishwa katika maisha yake, ugonjwa wa kichomi Alifariki mwishoni mwa usiku, saa hiyo hiyo, ambapo siku zote, baraka ya padre ilikuwa inamwondolea hali yake ya kukakamaa mwili. Padre huyo alikuwa Askofu Mkuu Petronelli Francesco, Machi 25, mwaka 1939 hadi tarehe 16 Juni, mwaka 1947. Luisa alibaki amekaa juu ya kitanda. Haikuwezekana kumnyoosha, na jambo la ajabu, mwili wake haukuwa na ukakamavu wa maiti, na hivyo uliendelea kuwa katika hali hiyo, kama ile uliokuwa nayo daima.
Mara tu habari za kifo cha Luisa zilipoenea, kama mafuriko kamili ya maji, jumuiya yote ya watu ilijimwaga katika nyumba yake, na ilikuwa lazima kutaka msaada wa polisi, ili kudhibiti kundi hilo la watu, ambalo usiku na mchana, lilienda kumwona Luisa, wanawake walimpenda sana, kwa mioyo yao yote. Sauti moja ilikuwa inasikika ikisema: “Luisa Mtakatifu amefariki?” Kwa kuweza kumudu watu wote, waliokuwa wakifika kumwona, ilibidi kibali cha uongozi wa serikali na wa kiafya, mwili ulibaki wazi kwa siku nne, bila dalili yoyote ya kuoza. Luisa hakuonekana
Kama amekufa, alikuwa amekaa juu ya kitanda chake, amevikwa nguo nyeupe; alikuwa kama amelala, kwa sababu, kama ilivyokwisha semwa tayari, mwili wake haukuwa na ukakamavu kama maiti, kwa kweli mtu aliweza, bila kutumia nguvu, kugeuza kichwa chake katika pande mbalimbali, kuinua mikono, kukunja viganja na vidole vyote, mtu aliweza pia, kuinua kope na kuangalia macho meupe yasiyofunikwa. Wengi walidhani kwamba alikuwa bado mzima, kama aliyekuwa katika usingizi mzito.Daktari mmoja aliyeitwa wakati wa kufa, baada ya kuchunguza vema maiti, alitamka kwamba Luisa alikuwa amefariki kweli kweli, na kwamba mtu alipaswa kufikiri juu ya kifo cha kweli, na siyo kifo cha kuonekana tu, kama watu wengi walivyokuwa wanafikiria.
Luisa alikuwa amethibitisha kwamba, alizaliwa kchwa chini, miguu juu, au katika hali isiyo ya kawaida, kwa hiyo, ilikuwa haki kwamba, kifo chake kingekuwa si cha kawaida pia, au kinyume na viumbe vingine. Alibaki amekaa, kama alivyoishi daima, na hivyo alipaswa kwenda makaburini hali amekaa, katika sanduku moja lilotengenezwa hasa kwa hali hiyo, lenye sehemu za ubavuni na za mbele zikiwa za vioo, kwa namna kwamba, aliweza kuonekana kwa kila mtu, kama malkia aliyeketi juu ya kiti chake, akiwa amevaa nguo nyeupe, na neno la FIAT kwenye kifua chake. Zaidi ya mpadre arobaini, wakuu na mapadre mahalia, walishiriki kwenye uwanja wa mazishi au maombolezo, masista upande wao, walimbeba kwa zamu katika sehemu ya mabegani; Kundi kubwa sana la wananchi lilimzunguka; barabara zilikuwa zimefurika kiasi cha kutoweza kufikiriwa; hata roshani na mahema ya nyumba yalikuwa yamejaa watu, na maandamano yalikuwa yakisonga mbele kwa shida kubwa sana. Ibada ya mazishi ya binti mdogo wa Utashi wa Mungu ilifanyika, katika Kanisa Mama la Jimbo zima. Watu wote wa sehemu ya Corato walisindikiza maiti hadi makaburini. Kila mtu alitaka kuchukua nyumbani kwake kumbukumbu ya maua, baada ya kugusa mati ambayo, baada ya miaka kadhaa, ilihamishwa na kupelekwa katika parokia ya Maria Mtakatifu wa Greca.
Mwaka 1994, Sikukuu ya Kristo Mfalme, katika Kanisa Mama, Mhashamu Askofu Carmelo Cassati, mbele ya umati mkubwa sana wa watu, na wawakilishi wengi kutoka nje, alifungua rasmi kazi ya kuanza kumtangaza kama nwenyeheri, Mtumishi wa Mungu, Luisa.
TAREHE MAALUM
1865: Luisa Piccareta alizaliwa tarehe 23 mwezi wa Aprili, Jumapili IN ALBIS, sehemu ya Corato (BA), na Vito Nicola na Tarantino Rosa, ambao walikuwa na watoto wa kike watano, yaani, Maria, Rachele, Filomena, Luisa na Angela. Saa chache baada ya kuzaliwa Luisa, baba yake alimfunika blanketi na kumpeleka katika Kanisa Mama, ili akabatizwe. Mama yake hakuwa na uchungu wa kumzaa; alizaliwa bila uchungu au maumivu.
187: Alipewa Y esu wa Ekaristi siku ya Jumapili IN ALBIS na siku hiyo hiyo alipewa Sakramenti ya Kipaimara na Askofu Yosefu Bianchi Dattura, Askofu Mkuu wa Trani.
1883: Akiwa na umri wa miaka kumi na minane, akiwa roshani nyumbani kwao alimwona Yesu amejikunyata chini ya msalaba ambaye alimwambia Luisa, “ROHO, NISAIDIE”. Tangu hapo, roho ya upweke, iliishi katika umoja wa kudumu wa mateso yasiyo elezeka ya Mchumba wake wa Kimungu.
1888: Alikuwa binti wa Maria na Mdominikani wa Daraja la Tatu na kuitwa Sista Magdalena.
1885 – 1947: Roho teule, mchumba wa Kimalaika wa Kristo, mnyenyekevu na mcha Mungu, alijaliwa na Mungu Karama za ajabu kafara asiye na hatia, kinasaumeme cha Haki ya Ki-mungu, kwa muda wamiaka sitini na miwili bila kukoma, ya kukaa au kulala kitandani, alikuwa Mtangazaji wa mbele wa Ufalme wa Utashi wa Ki-mungu.
4 Machi 1947: Akiwa amejaa mastahili, katika mwanga wa milele wa Utashi wa Mungu, alifunga kama alivyoishi, siku zake, ili akashangilie pamoja na malaika na watakatifu, katika utukufu wa milele wa Utashi wa Mungu.
7 Machi 1947: Masalia yake ya milele, kwa muda wa siku nne, yalikuwa yakipewa heshima na kundi kubwa sana la waumini, ambao waliingia nyumbani kwake, ili wamwangalie Luisa Mtakatifu, kwa mara ya mwisho, ambaye walimpenda sana kwa moyo wao wote. Mazishi yake, yalikuwa ni shangilio au shangwe ya kweli. Luisa alipita kama Malkia, akibebwa mabegani,katikati ya mabawa ya watu. Wahudumu wote wa Kanisa wenye madaraja au Makleri, Walei na Watawa walisindikiza maiti ya Luisa. Ibada ya mazishi ilifanyiwa katika Kanisa Mama, uongozi wote ukiwepo.Alasiri, Luisa alizikwa katika Kikanisa kidogo hisani cha familia ya Calvi.
3 Juni 1963: Masalia yake ya daima yalifukiwa moja kwa moja, katika Kanisa la Maria Mtakatifu Greca.
20 Novemba 1994: Kipindi cha Sikukuu ya Kristo Mfalme, Askofu Cassati, katika Kanisa Mama la Corato, mbele ya umati mkubwa sana wa watu, mahalia, na wa kutoka nje, alifungua rasmi kazi ya kumtangaza kama Mwenyeheri, Mtumishi wa Mungu, Luisa Piccarreta.
WAUNGAMISHI NA WASHAURI WA KIROHO
1. Padre Cosma Loiodice:Mmonaki na Muungamishi wa kwanza.
2. Don Michele De Benedictis : Muungamishi wa Luisa alipokuwa msichana mdogo sana,
aliyeteuliwa mwaka 1884, kama muungamishi wake rasmi kwa
amri ya Askofu Josefu B. Dottula.
3. Don Gennaro di Gennro : Paroko wa Parokia ya San Giuseppe, mwungamishi tangu 1898
hadi 1922, kwa utii, alimwamuru Mtumishi wa Mungu kuandika
yote, ambayo siku hadi siku Bwana alimfunulia Luisa.
4. Padre Hannibal Maria di Francia : Tangu mwaka 1919 hadi 1927, kwa amri ya Askofu
alikuwa ni muungamishi wake asiye wa kawaida, msomaji na
msahihishaji wa Kanisa wa maandishi ya Mtumishi wa Mungu;
alichapisha baadhi ya maandishi yake, ambayo kati yao ni ,
“Saa ya Mateso”.
5. Askofu Fernando Cento: Mjumbe wa Kitume na Kardinali wa Kanisa Takatifu la Roma.
6. Don Francesco De Benedictis : Muungamishi tangu mwaka 1922 hadi 1926, akiwa amemrithi
Don Gennaro di Gennro.
7. Don Felice Torelli : Paroko wa Parokia ya Santa Maria Greca.
8. Don Ciccio Bevilacqua : (Askofu) msaidizi wa Kanisa Mama, mwuungamishi wa mara
moja moja.
9. Don Luca Mazzilli : Msaidizi, muungamishi wa mara moja moja.
10. Don Beneditto. Calvi: Muungamishi wa kudumu au thabiti tangu mwaka 1926 – 1947, kwa
amri ya Askofu Mkuu Giuseppe (Josefu) Leo.
11. Don Peppino Ferrara : kwa mara kadhaa alikuwa msomaji Misa.
12. Don Vintantonio Patruno : Msomaji wa misa wa mara moja moja
13. Don Clemente Ferrara : Kasisi Mkuu na Kiongozi wa Misa wa mara moja moja
14. Don Cataldo Tota : Gombera wa Semirari ya Bisceglie na Paroko wa Kanisa la San
Francesco.
15. Askofu Michele Samarelli: Makamu wa Askofu wa Bari.
16. Askofu Ernesto Balducci : Makamu wa Askofu wa Salerno.
17. Askofu (Monsignori Luigi D’Oria) : Padre wa mambo ya kiroho wa Seminari ya Jimbo, au
Mkoa wa Molfetta na Makamu wa Askofu wa Trani.
Hata mapadri wengine wengi, watawa na wanajimbo, ambao hawako kwenye orodha hii, mara moja moja, walifika, kwa nia zao mbalimbali, nyumbani kwa Mtumish wa Mungu.
MAASKOFU
kumbukumbu zake).
Alikufa 16 Juni 1947, miezi mitatu baada ya kifo
Kitakatifu cha Luisa Piccarreta.
Mungu na akaruhusu kuenea kwa sanamu ndogo ya Luisa
kwa sala.
11. Askofu Carata Giouseppe:Mwaka 1971, mstaafu. Alitoa mwanzo kwa kibali cha sheria
ya Kanisa mwaka 1986 kwa Shirika la Utashi wa Kimungu,
katika sehenu ya Corato, baada ya kipindi cha miaka kumi.
Wakati huo huo, alito amri, akiwa amesukumwa na Kardinali
Palazzini, Msimamizi na Shirika kwa ajili ya kutaja watu kama
watakatifu, ya kukusanya ushahidi juu ya Mtumishi wa Mungu.
12. Askofu Cassati Carmelo: Mstaafu – Alifungua kazi au shughuli za kutajwa Mwenyeheri
Piccarreta, kwenye Sikukuu ya Kristu Mfalme, mwaka 1994.
13. Askofu Giovanni Battista Picchieri: Askofu Mkuu wa Wakati huo wa Trani. Yeye
aliombwa tena kuendeleza kazi ya kumtaja Mtumishi wa
Mungu, Luisa Piccareta Mwenyeheri.
ORODHA YA MAANDISHI YA LUISA PICCARRETA
Tarehe za maandishi ya Luisa Piccarreta kwa utii wa waungamishi wake na pia Luisa kwa maandishi yake, alipaswa kutegemea tu mamlaka ya Kanisa. Hasa au kwa kweli, shingo upande, akijiweka chini ya utii, alianza kuandika tarehe 28 mwezi Februari mwaka 1899.
JUZUU TAREHE
1-2 28 Februari – 30 Octoba 1899
3 1 Novemba 1899 - 4 Septemba 1900
4 5 Steptemba 1900 – 18 Machi 1903
5 19 Machi - 30 Octoba 1903
6 1 Novemba 1903 – 16 Januari 1906
7 30 Januari 1906 – 30 Mei 1907
8 23 Juni 1907 – 30 Januari 1909
9 10 Machi 1909 – 3 Novemba 1910
10 9 Novemba 1910 – 10 Februari 1912
11 14 Februari 1912 – 24 Februari 1917
12 16 Machi 1917 – 26 Aprili 1921
13 1 Mei 1921 – 4 Februari 1922
14 4 Februari - – 24 Novemba 1922
15 28 Novemba 1922 – 14 Julai 1923
16 23 Julai 1923 – 6 Juni 1924
17 10 Juni 1924 – 4 Agosti 1925
18 9 Agosti 1925 – 21 Februari 1926
19 23 Februari - – 15 Septemba 1926
20 17 Septemba 1926 – 21 Machi 1927
21 23 Februari - – 26 Mei 1927
22 1 Juni - – 14 Septemba 1927
23 17 Septemba 1927 – 11 Machi 1928
24 19 Machi - - 3 Octoba 1928
25 7 Octiba 1928 - 4 Aprili 1929
26 7 Aprili - – 20 Septemba 1929
27 23 Septemba 1929 – 17 Februari 1930
28 22 Februari 1930 – 17 Februari 1931
29 13 Februari - – 26 Octoba 1931
30 4 Novemba 1931 – 14 Julai 1932
31 24 Julai 1932 - 5 Mai 1933
32 12 Machi - – 10 Novemba 1933
33 19 Novemba 1933 – 24 Novemba 1935
34 2 Desemba 1935 – 2 Agosti 1937
35 9 Agosti 1937 – 10 Aprili 1938
36 12 Aprili - – 28 Desemba 1938
SURA YA PILI
UFALME WA UTASHI WA MUNGU
( Na sasa neno moja kwenu nyote mtakaosoma maandishi haya........)
Ninawasihi, ninawaomba mpokee kwa upendo kile Yesu anachopenda kutupatia, yaani Utashi au Mapenzi yake. Lakini, ili awape yake, anataka yenu, vinginevyo hataweza utawala huo. Kama mungefahamu ....... kwa upendo huu Yesu wangu anapenda kuwapa zawadi kubwa zaidi inayokuwa mbinguni na duniani ambayo ni Utashi wake.
Ah! Yesu alimwaga machozi mengi sana, kwa sababu aliona kwamba, kwa matashi yenu mnaacha alama za huzuni juu ya dunia yote, Je! Ninyi si wema, kiasi cha kuweza kufunza nia njema, na kujua sababu? Kwa sababu Utashi wake hautawali pamoja nanyi.
Ah! Jinsi Kristo anavyolia, anahema akikumbuka juu ya maangamizi yenu. Na muwezeshe Utashi wake utawale ndani yenu. Anataka mubadili bahati, yaani, kutoka kwa hali ya ugonjwa, muwe wazima, kwa ufukara muwe matajiri, kutoka kwa unyonge muwe wenye nguvu, kutoka kwenye hali ya ugonjwa, muwe wazima, kwa ufukara muwe matajiri, kutoka kwa unyonge muwe wenye nguvu, kutoka kwenye hali ya kubadilikabadilika, muwe imara, badala ya kuwa watumwa, muwe wafalme. Hapendi vitubio vikubwa, sala ndefu, wala kitu kingine; ila kwamba utashi wake utawale ndani mwenu, na wenu usiwe tena na nguvu. Msikieni Mungu, na mimi niko tayari kutolea maisha yangu kwa ajili ya kila mmoja wenu, kuvumilia mateso yoyote yale, ili mradi tu, mfungue milango ya mioyo yenu, na utashi wa Yesu wangu utawale na ushangilie juu ya vizazi vya wanadamu.
Sasa mtake wote kukubali wito wangu, njoni pamoja nami katika Bustani ya Aden, ambako asili yenyewe ilikuwa na mwanzo wake, ambako Uwepo wa hali ya juu sana ulimwumba mwanadamu, ambako ulimfanya kuwa mfalme, na kumpa ufalme wa kutawala, ufalme huo ulikuwa ulimwengu mzima, lakini fimbo yake ya kifalme, kofia yake, na amri yake vilikuwa vinatoka kwenye kiini cha moyo wake, ambako Fiat au NDIYO YA Kimungu ilikuwa imekaa, kama Mfalme Mtawala na alikuwa anafnya Ufalme wa kweli ndani ya mwanadamu. Mavazi yake yalikuwa ya Kifalme, yaking’aa zaidi kuliko jua, matendo yake yalikuwa ya kushangaza, na uzuri wake wa kuvutia sana. Mungu alimpenda sana, alifurahishwa naye, alimwita mfalme wangu mdogo na mwana. Yote yalikuwa ni furaha, sawa na yenye utulivu.
Mtu huyu, baba yetu wa kwanza, alijisaliti yeye mwenyewe, alisaliti ufalme wake, akifanya mapenzi yake, alimsikitisha Muumba wake, ambaye alikuwa amemwinua na kumpenda sana, na akapoteza ufalme wake, Ufalme wa Utashi wa Kimungu, ambamo alikuwa amepewa kila kitu. Milango ya Ufalme ilifunguliwa na Mungu akamrudishia ufalme, aliokuwa amepewa mwanadamu. Na kwa hiyo, sikilizeni siri yangu.
Mungu, katika kujirudishia ufalme wa utashi wa kimungu hakusema kwamba, asingempa tena mwanadamu ufalme huo, ila aliuweka akiba, akisubiri vizazi vijavyo, kwa kuushambulia kwa neema za kushangaza, na mwanga wa kupofusha macho, kwa kulea giza kwenye Utashi wa mwanadamu, ambao ulimfanya apoteze ufalme Mtakatifu vile na kwa talasimu (au aina ya uchawi) ya ujuzi wa kushangaza na wa kimuujiza ya Utashi wa Kimungu, kuyafanya yasikie haja ya hamu ya kuweka pembeni utashi wetu, ambao unatufanya tusiwe na raha, na kututupa katika Utashi wa Kimungu. Kwa hiyo Ufalme ni wetu, na hivyo jipeni moyo!
Fiati au Ndiyo ya Juu zaidi inatusubiri, inatuita, inatusukuma ili tuchukue hiyo Fiat kama mali yetu. Ni nani atakayekuwa na moyo wa kujikana mwenyewe, atakayekuwa mjanja kiasi cha kutosikia wito wake, na kutopokea furaha? Tuyaache matambara mabovu ya utashi wetu, mavazi ya matanga ya utumwa wetu, ambamo utashi huo umetutupa, na sisi tutavaa yale ya malkia, na tutajipamba kwa mapambo ya Kimungu!
Hivyo ninatoa wito kwa wote: nisikilizeni, fahamuni, mimi niko kadogo, kadogo zaidi kuliko viumbe vingine vyote.... nitajiweka mahali pawili kwa wakati mmoja katika Utashi wa Mungu pamoja na Yesu, nitakuja kama katoto kadogo ndani ya tumbo lenu, na kwa vilio na kelele nitagonga kwenye mioyo yenu, ili niwaombe, kama ombaomba mdogo, matambala yenu, mavazi ya msiba, Utashi wake, awape Ufalme wake, furaha yake, weupe wa nguo zake za kifalme.
Kama mngalijua maana ya Utashi wa Mungu! Ndani mwake kuna Mbingu na nchi; kama tuko pamoja na Utashi huo, kila kitu ni chetu, kila kitu ni kutoka kwetu; kama hatuko pamoja na Utashi huo, kila kitu kinapingana na sisi; na kama tuna kitu chochote, sisi ni wezi wa kweli wa Muumba wetu, na tunaishi kwa njia ya ulaghai na unyang’anyi.
Hivyo, kama mnataka Utashi huo, someni kurasa hizi: yaani, humo mtakuta mafuta au dawa ya vidonda, ambavyo Utashi wa mwanadamu, bila huruma, umetupatia, hewa mpya yote ya kimungu, uzima mpya wote wa mbinguni, mtasikia Mbingu ndani ya mioyo yenu, mtaona peo mpya za macho, majua mapya na mara chache mtamwona Kristo mweye uso uliolowa kwa machozi, unaotaka kuwapa Utashi wake. Yeye analia kwa sababu anapenda kuwaona ninyi mkiwa na furaha, na anapowaona mkiwa bila furaha, humezea, akapumua, na kuombea furaha ya Watoto wake; na akiwaomba Utashi wenu ili awaondoe kutoka kwenye masikitiko, anawapa Utashi wake, kama uthibitisho wa zawadi ya Ufalme wake.
Kwa hiyo, ninawaomba wote; na ninafanya au ninatoa wito huo, pamoja na Yesu, na machozi yake yote, na pumzi zake zenye kuangaza au kuwaka, na Moyo wake unaounguza, ambao unakutaka kutoa Ndiyo au Fiat yake. Tumetoka ndani ya Ndiyo au Fiat hiyo, tulikuwa na uzima, ni haki, ni lazima kwamba tutarudi ndani ya Ndiyo au Fiat hiyo, ndani ya urithi wetu mpendelevu usio na mwisho. Na kwa mara ya kwanza, ninatoa wito, kwa Baba Mtakatifu, Papa, wawakilishi wa Kanisa Takatifu, na hivyo, Wawakilishi wa Ufalme wa Utashi wa Mungu.
Kadogo huyu anaweka ufalme huu chini ya miguu yake mitakatifu, hadi amfanye amtambue; na kwa sauti yake ya kibaba na yenye mamlaka, awaite watoto wake kuishi katika Ufalme Mtakatifu vile. Fiat yake ya juu zaidi kuliko vyote, aiwekeze, na atengeneze jua la kwanza la Utashi wa Kimungu ndani ya Mwakilishi wake duniani; na kwa kutengeneza uzima wake wa mbele ndani yake.Yeye, ambaye ni Mkuu wa Kanisa, aeneze mionzi yake isiyo na mipaka duniani kote, na kwa kushinda vitu vyote kwa uzuri wa mwanga wake, atengeneze zizi moja peke yake na mchungaji mmoja!
Wito wa pili ninautoa kwa Mapadri wote. Nikiwa nimeanguka chini ya miguu ya kila mmoja wao, ninaomba, ninasihi, ili wapende kujua Utashi wa Kimungu. Na ninasema au ninawaambia; msemo wa kwanza, chukueni tendo la kwanza kutoka kwake, yaani, Utashi wa Kimungu; hasa jifungieni ndani ya Ndiyo –Fiat, na mtasikia jinsi uzima wake ulivyo mtamu na mpendwa; kutoka kwake mtateka shughuli zenu zote, mtasikia ndani mwenu nguvu ya kimungu, sauti ambayo daima inazungumza, ambayo itawaambia mambo ya kushangaza ambayo hamjapata kuyasikia, mtasikia mwanga unaoshinda kila ubaya kwa mwanga wake,na kwa kugusa watu, utawapeni utawala juu yao. Ni Kiasi gani mnajichosha bila faida, kwa sababu hakuna Utashi wa Mungu! Mmevunja mkate kwa watu usio na chachu ya Ndiyo-Fiat, na hivyo, wao kwa kuula wameuona ni mgumu, karibia usioweza kuyeyushwa tumboni; na bila kusikia maisha ndani mwao, hawajiweki kabisa chini ya mafundisho yao. Kwa hiyo, uleni mkate huo wa Fiat ninyi, kwa namna hiyo, mtatengeneza, pamoja na watu wote, maisha yake na Utashi mmoja tu.
Wito wa tatu ninatoa kwa ulimwengu wote, kwa kaka zangu wote na dada zangu na watoto wangu. Mnafahamu kwa nini ninawaiteni wote? Kwa sababu ninataka kuwapa wote uzima wa Utashi wa Kimungu. Utashi huo wa Kimungu ni zaidi ya hewa ambayo wote tunaweza kuivuta, ama kama jua, ambako sisi sote tunaweza kupata mema ya mwanga wake; na kama pigo la moyo ambalo linataka kudunda ndani ya kila mtu; na mimi, kama mtoto mdogo wa kike, ninapenda, ninapumua, ili mchukue uzima wa Ndiyo-Fiat. Oo!! Kama mungejua ni mema mangapi mungepata, mungeweka uzima ili muufanye utawale ndani mwenu wote!
Kadogo huyu anataka kusema siri nyingine, ambayo Kristo amemwaminisha, na ninawaambia, hadi mnipe Utashi wenu, na kwa kubadilishana, mtapata- au muweze kupata ule wa Mungu, ambao utawafurahisha moyoni na mwilini.
Mnapenda kufahamu kwanini ardhi haizai? Kwa nini katika sehemu nyingi za dunia, yenye matetemeko ya mara kwa mara, ardhi hufungua na kufunga ndani ya tumbo lake miji na watu? Kwa nini upepo, maji hufanya dhoruba na kuharibu kila kitu? Kwa nini kuna maovu mengi namna hii, ambayo ninyi nyote mnayafahamu?
Kwa sababu viumbe vina Utashi wa Kimungu, unaovitawala, na hivyo, vina uwezo na vinatawala, vinaheshima zaidi kuliko sisi, kwa sababu sisi tumetawaliwa na utashi wa kibinadamu, na kwa hiyo, tumedharauliwa tu, wadhaifu na tusiojiweza. Kama kwa bahati yetu tungefunga utashi wa kimungu, na sisi sasa tungekuwa ndugu wa viumbe vyote, ambvyo, si tu, havitatusumbua tena, ila vitatuwezesha kuvitawala, na sisi tutafurahi wakati huo na milele.
Je, mumefurahi? Kwa hiyo, fanyeni hima sikilizeni huyu maskini kadogo, ambaye anawapenda sana. Na mimi sasa nitafurahi, nitakapoweza kusema kwamba, kaka zangu na dada zangu wote ni Wafalme na Malkia, kwa sababu wote wana uzima wa Utashi wa Kimungu!
Jipeni moyo, jibuni wito. Ndiyo, ninahisi wote kwa pamoja mtaweza kunijibu; na zaidi sana, kwa sababu si mimi peke yangu ninaye waita, ambaye ninawaomba, akiwa ameungana na mimi anawaita, kwa sauti nyororo na ya kuvutia, Yesu wangu mwema, ambaye,mara nyingi, pia akiwa analia, anatwambia: Twaeni, kwa maisha yenu, Utashi wangu; njoni katika Ufalme wake. Jueni kwamba mtu wa kwanza kusali kwa Baba wa Mbinguni, ili Ufalme wake uje, na kwamba Utashi wake ufanyike Mbinguni kama vile duniani, alikuwa Bwana wetu, aliposema Baba yetu, na kwa kueneza kwenu sala yake, alitoa wito kwetu, na kuomba ili sote tuombe,”MAPENZI YAKO YAFANYIKE MBINGUNI NA DUNIANI.” Kwa hiyo, kila wakati msalipo Baba yetu, Yesu hushambuliwa na hamu kubwa sana ya kupenda kuwapa Ufalme wake, Utashi au Ndiyo yake, ambayo anahitaji kuisema pamoja na sisi: yaani, Baba yangu, ni mimi ninayekuomba, kwa ajili ya watoto wangu, fanya haraka.” Kwa kuwa na ninyi mnamwomba katika Baba yetu... Je, kwa hiyo, msingependa sana vile?”
Neno la mwisho. – Mnaweza kujua kwamba, Mtoto Mchanga huyu wa kike, kwa kuona hamu, furaha isiyo na kifani, machozi ya Yesu, mwenye tamaa ya kuwapa Ufalme wake, Utashi au Mapenzi yake, ana hamu kubwa sana, pumzi kubwa sana, wasiwasi mwingi, wa kutaka kuwaona ninyi nyote katika Ufalme wa Utashi wa Kimungu, wote wenye furaha kiasi cha kumfanya Yesu acheke, ambaye, kama hafaulu kwa sala, kwa machozi, atatafuta kutufanya tufaulu kwa nia zake zilizo karibu sana na Yesu na karibu nanyi pia. Kwa hiyo, msikilizeni kadogo huyu mdogo msimfanye tena, apige kite, mwambieni, aksante: “iwe hivyo..... iwe hivyo... sote tunapenda ufalme wa Utashi wa Kimungu – Ndiyo – Mapenzi yako yafanyike.”
Sala nyingine zisizosahihishwa
Nimejifungia ndani ya Utashi wako
Yesu wangu, ninajifungia ndani ya Utashi wako hadi nipumue kwa Pumzi yako, ili nipumue kwa pumzi ya wote na nizigeuze ziwe busu nyingi zenye kishindo.
Ninafanya pigo la moyo wangu, lipige ndani ya Utashi wako, kwa kukwambia katika mapigo yote ya mioyo nikisema, “Ninakupenda Ninakupenda, na nikijisogeza ndani ya Utashi wako, ninakupa mafumbato ya watu wote, mpaka mtu yeyote, akiwa ameng’ang’ania kwako, akifumbatwa na fumbato lako, asiweze kukukosea, na watu wote wakupende, wakuabudu, wakubariki, na wote wafanye utashi au Mapenzi yako.
Wewe ni kiongozi wangu: Yesu wangu mwema, nifungie ndani ya Utashi wako, mpaka nisione, nisisikie, nisiguse isipokuwa Utashi wako, na kwa uwezo wako, nifanyike mtakatifu. Yesu, katika matendo yangu, kwa kujaza Mbingu na nchi kwa uzima wa kimungu. Mama Malkia, uwe wewe kiongozi wangu, mwalimu wangu, na usiniruhusu nipumue hata pumzi moja bila Utashi wa kimungu.
Twaa utashi wangu: Yesu wangu, nipe Utashi wako na uchukue wangu, mpaka niwe mtakatifu kwa utakatifu wako, nipende kwa Pendo lako, nipumue kwa moyo wako, nitembee kwa hatua zako, nipumzike kwa utulivu wako, na kwa neno langu, nitengeneze Yesu ndani ya mioyo ya wale wanaonisikiliza.Mama Malkia, nifunike chini ya vazi lako, ili unifunze nikiwa nimelindwa na watu dhidi ya kila kitu.
SURA YA TATU
Mwanamke Mwenye kifafa aponyeshwa
Shangazi Rosalia, aliyezaliwa tarehe 4 mwezi Aprili mwaka 1898, wa mwisho kati ya watoto wengi, kama alivyosema bibi yangu, alikuwa mtoto wa kike peke yake, ambaye hakuwa na bahati katika familia, kwa kuwa chini ya kipeo cha kifafa. Isitoshe, yeye huyo huyo, kwa sababu ya ajali ya kawaida, pingili za kidole cha kati, cha pete na kile kidogo cha mkono wa kushoto, vilikatika. Bibi yangu, akiwa na matumaini ya kupona, alipeleka Rosaria kwa Luisa,kwenye makao yake ambako kikundi cha wasichana kilikuwa kinaenda kufundishwa ufundi wa kutarizi kwenye bahati nasibu. Luisa aliomba awekwe kati yao, kwa namna kwamba angeweza kujifunza kazi hiyo. Shangazi Rosalia, wakati huo ndo alikuwa amefikisha umri wa miaka tisa, hata kama alionyesha kuwa mkubwa zaidi. Tuko katika mwezi wa januari mwaka 1907, ilikuwa ni siku ya baridi sana na mvua. Luisa Mtakatifu. Kadogo au Piccarreta hakuwa tu mwanamke wa maisha matakatifu, akiheshimiwa na wote, ila pia alikuwa ni mtendaji wa kike wa jamii. Hasa; alikuwa amejenga nyumbani kwake shule ya ufundi wa kutarizi kwenye bahati nasibu, ambayo siku zile ilikuwa na maendeleo makubwa ya kijamii kwa wasichana wengi, waliokuwa wanaenda nje ya mazingira ya nyumbani na kilimo.
Hivyo ndivyo mkutano ulivyotokea ...... Ilikuwa inakaribia saa nne, bibi yangu alipoenda pamoja na shangazi nyumbani kwa Luisa, iliyokuwa katika barabara ya Nazario Sauro, iliyoitwa barabara ya Hospitali. Mama ya Luisa alikuja kufungua mlango, ambaye alikuwa ameendelea mbele kwenye umri, na ambaye alijiburudisha kwa mazungumzo au pororojo na bibi yangu, akimwuuliza habari za ndugu zetu fulani.
Baada ya mazungumzo, mama ya Luisa aliwasindikiza wageni wawili hao, katika chumba kidogo cha binti yake, ambaye akiwa kitandani alikuwa anawapa wasichana mafunzo ya kutarizi.
Angelina, dada ya Luisa, aliwatoa nje wasichana waliokuwa wanatarizi, akachukua kiti bibi yangu alichokuwa amekalia, na wawili hao wakaanza mazungumzo.
Huu ndio ulikuwa ushuhuda wa shangazi yangu. “Wote wawili walizungumzia maswala au hoja mbalimbali, ambazo mimi sizikumbuki vema, kama marafiki wazee wa zamani, ambao walikuwa hawajakutana kwa muda kitambo. Mwisho, mama yangu alimbusu Luisa na kuondoka. Nilihisi kwamba hawa wanawake wawili walizungumza pia juu yangu, na kwamba Luisa alikuwa ameafikiana na ombi la mama yangu. Nilipobaki peke yangu na Luisa, alinitazama kwa makini sana. Kwa mtazamo au kwa jicho la upole, kama vile angependa kunitia moyo. Mimi sikuhisi lolote lile, ambalo lingeweza kunitokea,yaani, kubaki karibu naye, bila kukoma, kwa miaka arobaini.Miaka kadhaa baadaye, shangazi yangu alishambuliwa na kipeo cha ghafla cha kifafa, wakati, alipokuwa anapewa misingi ya kwanza ya mafunzo ya kutarizi ya bahati nasibu. Shangazi yangu hakusimulia hata siku moja tukio hilo, kwa kuwa alikuwa kidogo, mtumwa na mkimya juu ya kile kilichomhusu Luisa, na mara chache sana, alizungumza habari za nyumbani. Jambo hilo mimi nilisimuliwa na mama yangu, ambaye alikuwa amelifahamu kutoka kwa rafiki yake wa kike, aliyekuwepo wakati wa tukio hilo.
Mara tu, shangazi yangu alipoanguka chini, ulimi nje, povu lote lililomtoka likiwa ni lile la kifafa, wasichana waliokuwepo waliogopa sana na kukimbia mbali, wakati huo huo shangazi yangu alisaidiwa na Angelina, dada yake na Luisa. Wakati huo, Luisa hakuwa na wasi wasi hata kigodo, kama vile tukio hilo halimhusu kabisa, akiwa naendelea kufanya kazi yake. Msichana mmoja, ambaye licha ya hofu aliyopata alibaki katika nafasi yake, anashuhudia akisema: “Luisa,jinsi alivyomwona Rosaria ameanguka chini, aliinua macho yake juu mbinguni na kusema maneno haya: “Bwana, kama umemweka karibu na mimi, ninapenda apone.” Na akaendelea na kazi yake. Kwa sababu ya ghasia kubwa, hakuna aliyeipa heshima au kujali sala ya Luisa. Hiyo sala iwe ya kweli au hapana, tangu wakati ule shangazi Rosalia, hakusumbuliwa tena na kipeo hicho cha kifafa. Yeye aliishi na kufikia umri wa miaka themanini, na akauawa na Kipeo cha Ugonjwa wa kisukari, ndivyo ilivyogunduliwa baada ya kumpima. Ugonjwa wake ulikuwa wa siku moja na nusu.
Kengele ndogo ya Mfarakano
Shangazi Rosalia mumilikaji wa mambo ya familia hasa alikuwa amekataa nusu ya faida zilizopatikana, ambazo ziliweza, kwa enzi hizo, kufikiriwa zilikuwa zinamhusu, kwa upendeleo wetu, kwa sababu tulikuwa ni familia moja ya watu wengi, watoto wa kiume sita, wote wanafunzi, karibu kila siku, alikuja kula nyumbani kwetu, na alijisikia kuwa bi mkubwa wa hali hiyo. Kazi aliyokuwa anafanya shangazi nyumbani ilikuwa nzuri sana, hasa katika kushughulikia mambo ya nyumbani; yaani, alikuwa anasaidia kupika, kutayarisha meza, na alisaidia kuondoa vyombo kabla ya kuondoka.
Mchango wake huu ulithaminiwa sana, kwa sababu mama yangu alikuwa mwalimu, na sisi sote wanafunzi, na tuliweza, kwa shida sana kusaidia kazi za nyumbani. Mara chache hizo, ambapo shangazi Rosaria alikuwa haji, kila kitu kivurugika na kufanyika kwa haraka. Ninakumbuka kwamba, tulipokuwa tunarudi kutoka shuleni, tulimkuta shangazi Rosaria, daima tayari kutuhimiza tunawe mikono, na kufanya ishara ya msalaba, kabla ya kuanza kula chakula cha mchana.
Wakati mwingine, lakini, alionyesha ishara ya ajabu – isiyo ya kawaida, ambayo ilitufanya tugune, na kwa namna ya pekee, mama yangu. Namna ya kutenda, tuliiona kama ya ujeuri na yenye kupambanisha au changamoto, kama vile alitaka kuthibitisha kuwa, yeye ndiye alikuwa bi mkubwa wa nyumba. Yote hayo yalitegemea pia, tabia yake thabiti na isiyotegemezi, ambayo kwa shida sana ilikubali kuaminiwa.
Uwepo wake ulileta ndani ya kila mtu, aina fulani ya mfadhaiko, hakuna aliyethubutu nyumbani kutamka maneno, ambayo hayakuwa sahihi, na kwa shida sana, tulimpenda; hata siku moja hakutupatia zawadi ndogo ndogo au fedha. Alipatikana tu kama tulionyesha nia ya kuungama au kwenda kanisani, hasa kwenye sala za jioni, ambako yeye hakukosa hata siku moja. Alikwenda mara nyingi katika parokia ya Maria Mtakatifu wa Grecia, na nafasi yake ilikuwa ndani ya Kanisa ndogo ya Sakramenti Takatifu sana, akipiga magoti katika pembe ile ile. Tulipokuwa tukimtafuta kwa ajili ya kazi fulani za nyumbani au familia, kama hakuwa nyumbani kwa Luisa, tulimkuta kwenye nafasi yake ya kawaida Kanisani, akipiga magoti.
Siku moja mimi nilimwambia: “Je, magoti hayakuumi?” Alinichekea tu na wala hakujibu swali langu, ila aliongeza kusema: “Katika au mahali hapa, Luisa alikuwa anapiga magoti alipokuwa anaweza kwenda Kanisani. Ni mahali hapa ambapo Luisa alikuwa anazungumza na Yesu.”
Namna yake hii ya ajabu ya kutenda , ilikuwa inasumbua, na kwa sababu ya aina hii, maneno yake fulani mazito sana, aliyasema nyumbani kwetu. Sababu za ugonvi katika familia, hasa kati ya shangazi na mama yangu, ilikuwa kama ifuatavyo:
Mara nyingi, alipokuwa anakula, shangazi aliinuka haraka, akavua aproni na kuondoka.
Wakati mwingine, alipokuwa akijadili mambo muhimu ya kifamilia, alikatisha mazungungumzo yake na kupotea. Namna yake hii ya kutenda, ilikuwa inamwacha kila mtu amenyamaza, kwa sababu yeye hakuwa na hoja yoyote ya kueleweka. Kwa hiyo shangazi Rosaria alikuwa anafikiriwa mwanamke bandia na mnafiki, na mama yangu alihusisha tabia ya namna hii na kiburi chake. Ila baba peke yake, ambaye alimpenda sana dada yake, alitunza usawa na akamtetea daima, na hivyo, kuchochea hasira za mama yangu, ambaye alijisikia kuudhika kwa kutoheshimiwa vilivyo, jambo ambalo aliliona kwa shangazi yangu.
Sisi watoto tulikuwa tunafanya kwaya, na mama na shangazi Rosaria alikuja kwetu, akionekana kama kondoo mweusi wa familia yetu, chombo cha masimango yetu. Uingiliaji kati ya mama zetu ulikuwa wa lazima kwa ajili ya kutuliza jazba yetu isiyo na busara. Licha ya hayo yote, mama yangu alikuwa na heshima kubwa kwa shangazi Rosaria, na alitushauri akisema: “Kumbukeni kwamba, yeye daima ni roho iliyowekwa wakfu.”
Labda kwamba, siku moja baada ya shangazi Rosaria kufika nyumbani, kama vile hakukuwa na jambo lolote lililotokea, na alikuwa hajibu kitu kwa maelezo, ambayo mama yangu alikuwa anauliza, juu ya mwelekeo wake.
Kwa upande wa mtazamo wa padre, shangazi sasa alipokuwa mzee zaidi, na akizungukwa na heshima ya familia, nilimwuuliza sababu ya namna yake ya kutenda. Aliniuliza: “Je, unataka kweli kujua sababu hiyo? Inakupendeza?” Nilijibu, “Ndiyo.”
Hivi, ndivyo alivyoanza kusema: “Mimi niliteseka sana kwa kutofahamika kabisa, lakini hayo yalikuwa ni majaribu makubwa sana, ambayo Bwana aliniweka chini yake, ili nistahimili kuwa mlinzi wa Luisa. Yeye alitumia saa nyingi sana za siku nzima, katika kusali. Mimi nilihisi ni lini alikuwa anapenda kuachwa peke yake, na bila kuniambia kitu, mimi nilikuwa ninainuka kutoka kazini kwenye bahati nasibu, niliondoa mikononi mwake mchezo huo wa bahati nasibu, niliiweka juu ya meza, niliwaondoa watu wote kutoka chumbani mwake, nilifunga kamba ndogo za kitanda chake, kisha nilifunga chumba chake, na kazi iliendelea katika ukimya katika chamba jirani. Saa nyingi zilikuwa zinapita, na nilipokuwa ninasikia kengele ya mlango, mimi peke yangu niliingia chumbani kwa Luisa, nilifungua kamba za kitanda, nilirudisha chombo cha bahati nasibu mikononi mwake, kwa namna kwamba, waingiapo, waliweza kumkuta kama walivyomkuta, makini kwa kazi. Hata asubuhi, nilipokuwa bado kitandani, mimi peke yangu nilisikia kengele ya mlangoni, wakati mwingine, karibu na saa tisa au saa kumi. Dada yangu, Angelina, alikuwa ananung’unika kwa sababu, alikuwa akiamka kutoka usingizini aliposikia mimi ninaamka. Nilikuwa ninamkuta kama amekufa, akiwa bila ishara yoyote ya maisha; bila kujitikisa. Nilimtengeneza nywele zake, mito ikiwa nyuma ya mabega yake, ambayo mara nyingi nilikuwa ninaikuta ikiwa imeanguka chini. Ni jambo la kukumbuka kwamba, mito hiyo mitatu, ilikuwa inawekwa nyuma ya mabega ya Luisa, lakini Luisa alikuwa haiegemei hata siku moja, nilifanya kazi tu kufunika hewa tupu kati yake na sehemu ya juu ya kitanda. Baada ya kumweka sawa Luisa, nilitayarisha Altare kwa ajili ya Misa Takatifu, Padre alipokuwa anafika kwa ajili ya kusoma Misa, nilimruhusu yeye tu kuingia ndani ya chumba. Alimfanyia ishara ya Msalaba mwilini mwake na kumrudisha tena katika maisha haya. Baada ya kurudi katika hali ya kawaida. Luisa, wengine wote waliingia katika kuhudhuria kwenye Misa Takatifu, akiwemo mtumishi wa Misa, ambaye hakuweza kukosa. Luisa alihudhuria Misa Takatifu, kama vile alikuwa amepagawa kwa furaha kuu; kwa ibada kuu sana akijibu sala kwa kilatini sahihi kabisa. Baada ya komunio, wote waliondoka, wakati Luisa alikuwa anazama katika kushukuru kwa kina kikubwa sana na kirefu, kwa muda wa saa kadhaa. Karibia saa tatu asubuhi alipiga kengele, na sisi tukaingia chumbani mwake, na yeye alianza kazi yake ya kutarizi kwenye bahati nasibu. Mimi nilikuwa ninafanya kazi karibu na Luisa, na tulikuwa tunatumia mashine zile zile za kushonea, pamoja na uzi ule ule na vidonge au vigurudumu vilevile, na nilikuwa ninasahihisha kazi za Luisa, kwa sababu zilikuwa kidogo zimelegea, kwa kuwa hakuwa na nguvu ya kuvuta nyuzi, kwa sababu, ya maumivu aliyokuwa anasikia, katika mikono yake, kwa sababu ya makovu aliyokuwa nayo.”
Hapo mimi niliingilia kati na nikasema: “Lakini, mimi sijaona hata siku moja makovu au madonda hayo katika mikono yake.” Alinijibu akisema: “Bila shaka, kwa sababu yalikuwa ndani na ni mimi peke yangu na watu wengine wachache, tulikuwa tumeyaona. Kati ya watu hao ni waungamishi wake na dada zake Cimadomo, na inaonekana pia, mpwa wake, Josefina. Kwa kweli, kama mtu alishika mkono wa Luisa na kuulekeza kwenye jua, tundu la ndani lilionekana. Mara nyingi, ilipokuwa usiku ninaingia chumbani kwake, nilikuwa ninamkuta ameenea damu, tangu miguuni, mikononi, na ubavuni, damu ilikuwa inatiririka, kiasi kwamba, ililowanisha blauzi yake aliyokuwa anavaa, na kitandani. Wakati mwingine, damu ilifika hadi chini sakafuni. Si tu mwili wake, lakini pia kichwa na uso vilikuwa vimejaa damu: alionekana kama mtu aliyesulibiwa msalabani. Safari za kwanza mimi nilikuwa ninasisimukwa mwili, nikiamini kuwa amekufa kwa kupungukiwa au kuishiwa damu, na nilikimbia kuleta taulo ili nimsafishe, lakini nilipokuwa ninarudi nilimkuta amesafishwa mwili mzima, isipukuwa shuka zake. Kila kitu kilikuwa kimetoweka. Tukio hilo lilikuwa linatokea marambili au mara tatu kwa mwaka.”
Nilimwambia, “lakini hujapata kusimulia tukio hilo?” Hapana, alinijibu, Don Benedetto Calvi peke yake, ndiye alifahamu. Alinikataza kabisa nisisimulie tukio hilo na akasema kwamba, angenikatalia maondolea ya dhambi, kama kwa bahati mbaya, ningekoswa uangalifu wa kusimulia jambo hilo, kwa mtu yeyote, Wewe ni peke yako unayelijua, na ninatumaini kwamba, hatalichukulia vibaya.”
Kisha alinyamaza na kuendelea kusema: “Ninakusihi usisambaze jambo hili.” Alinipa mawazo kwamba alikuwa anajuta kwa sababu ya kulisimulia jambo au tukio hilo. Hasa, ilikuwa ni mara ya kwanza kwake kusimulia jambo hilo, Hili, ni kati ya matukio mengi yanayohusu maisha ya Luisa, yaliyobaki bila kujulikana.
Shangazi, baada ya kusimama kidogo alianza tena kusema: “ Kwa kawaida, Luisa alikuwa anafanyakazi peke yake, kwa ajili ya makanisa,alitengeneza na kutunza kwenye bahati nasibu, vitambaa vya mezani kwa aljili ya Altare, kanzu na suplisi kwa ajili ya mapadri.” Wakati mwingine, baada ya kuombwa sana, alihifadhi pale kazini matandiko ya kitandani kwa ajili ya maarusi vijana. Luisa alikuwa na tabia moja dhaifu kwa ajili ya kutakatifuza familia, na maarusi wengi vijana, waliokwenda kwake kwa ushauri. Alifanya mambo mengi sana mema, na kuokoa familia nyingi sana kutoka kwenye uharibifu. Luisa alipokuwa anajifungia katika sala, mimi nilikuwa ninatoka nje ya chumba, na niliporudi muda mfupi baadaye, alipiga kengele, ambayo nilikuwa siijali sana. Iliponibidi Kujitenga, kwa muda wa siku kadhaa. Yosefu mwipwa wake, alikuwa anachukua nafasi yangu. Lakini, wakati mwingine, nilipokuwa mbali nyumbani au Kanisani, au kwa rafiki zangu fulani, nilikuwa ninasikia kengele ikilia niliacha kila kitu, hata chakula cha mchana na kukimbia haraka kwa Luisa. Kwa namna yangu hiyo ya kufanya, nilifikiriwa kuwa mtu wa ajabu, si tu na familia, lakini pia na watu wa nje. Sikuweza kutoa maelezo kwa mlio wa kengele niliusikia mimi tu, na kama ningemweleza mtu mwingine, angenifikiria kuwa mwenda wazimu, na mwenye maono; jambo ambalo lilinifanya ninyamaze, na waliponiuliza sababu ya kuwa na mwelekeo wa aina hii, daima nilitafuta namna ya kubadilisha mazungumzo, nikijisingizia kama vile sikusikia. Yote hayo, yalinipa mateso makubwa sana. Mara nyingi, baada ya safari ya kuchosha, nilimkuta Luisa akisali. Nilimuuliza: --“Nani aliyekuwa anapiga kengele?”
- Alijibu: “Sijui, ni nani huyo?
- Na Luisa alikuwa anasema nini?”
- “Hakusema kitu”
- Na wewe, ulikuwa unafanya nini?
- Mimi nilipiga magoti karibu na kitanda chake nikawa ninasali”
- Lakini wewe hukuona kitu wakati wa sala ya Luisa? Je, ni kweli kile alichokuwa anasema juu
ya Luisa, kwamba mara nyingi, alijikuta akining’inia hewani?”
- “Siwezi kuzungumza juu ya mambo haya, daima Luisa alinikataza ni siseme kitu. Muungunishi tu ndiye alifahamu yote na alikuwa chombo cha kutunzia matukio yake yote yasiyo ya kawaida. Luisa kama upande wake, daima hakuruhusu hata neno dogo sana. Kila kitu kilipaswa kuwekwa chini ya mamlaka ya padre, na peke yake aliweza kusema kama,matukio ya aina hii yaliweza kusambazwa au kutangazwa. Luisa hakufanya wala kuandika kitu bila ruhusa ya muungamishi, alikuwa chini ya mamlaka ya Kanisa kiasi kwamba, hakukuwa na kitu kilichopaswa kujuliwa au kuandikwa na kutangazwa, bila kibali cha Kanisa lile lile. Ni katika mstari huu kwamba, mtu aliweza kufahamu kila kitu juu ya Luisa. Kila kitu kimeandikwa katika maandishi yake. Mimi niliongeza: “Lakini maandishi yake hayawezi kueleza yote juu ya maisha yake, kwa sababu maisha ya Luisa ni magumu sana kuyaeleza. Alinijibu akisema,” Hii ni kweli, Ningeweza kusema mambo ambayo hakuna mtu anayeyafahamu.
“Na Kwa nini unakuwa mgumu kusema?” Kama Luisa angekuwa amependa kwamba yajulikane, angeyaandika au kanisa lingemwamuru ayaandike; ni wazi kwamba matukio fulani, yaliyothibitishwa, ambayo kwayo mimi na watu wengine tulikuwa mashahidi, hayafai kwa kutakatifuza roho za watu. Bwana ameruhusu kwamba, kila kinachofaa kwa Kanisa na kwa ajili ya roho kingejulikana, mengine yaliyobaki hayasaidii kitu. Kwa kusema hivyo, inaonekana ninakufuru urafiki ambao ulikuwa umejengwa kati ya Mungu na Luisa, wanadamu wasingeuelewa. Ujumbe aliotuachia Luisa unazidi nafsi yake mwenyewe. Luisa alitaka kwamba, Mungu peke yake ndiye alipaswa kuwa na sifa yote na utukufu, na nafsi yake ilipaswa kupotelea hewani, kwa sababu hiyo, alipenda upweke, kimya, na alionyesha kusumbuliwa sana, alipoona kwamba, nafsi yake ilikuwa ni jambo la heshima, upande wa watu.” Kwa sababu walimwona kama mtu mmoja maskini na mgonjwa, mhitaji wa kila kitu. Mimi na wengine tulifahamu vizuri kabisa kwamba, Luisa hakuhitaji chochote kile, na sisi tulipaswa kuwa walinzi wa fumbo lake. Mara nyingi, asubuhi, nilikuwa ninamkuta Luisa kila kitu kimepangwa, Altare ikiwa imetayarishwa kwa ajili ya Misa Takatifu, na mishumaa imewashwa.”
- “Na yote hayo yalitokeaje, iwapo Luisa hakuweka hata siku moja miguu yake chini, kwa
karibia miaka sabini? Lakini, una uhakika na kile unachokisema?”
- “Hakika kabisa! Kwa sababu mimi tu nilikuwa ninaingia chumbani mwake.”
- “Hukupata kuulizwa au kuombwa utoe maelezo yoyote?”
- Nimefikiri kwamba, malaika walikuwa wanamhudumia, hasa Malaika wake mlinzi ambaye kwake alikuwa na ibada kubwa sana. Mara nyingi, chumba chake chote kilinukia na kutoa harufu nzuri sana,
- “Je wengine walikuwa wanasikia harufu hiyo nzuri ya manukato”
- “Ndiyo, wote waliokuwa wanahudhuria Misa Takatifu. Ninakumbuka kwamba, safari moja Don Cataldo De Benedictis, aliyekuwa amekuja kusoma Misa Takatifu, Muungamishi wake bila kuwepo, aliniambia”:
- “Msiweke manukato chumbani, vinginevyo nitatoka nje kichwa kinanigonga”
- Mimi nilimhakikishia kwamba, hakuna mtu aliyeweka manukato,lakini hakunisadiki.
- Je ni kweli kwamba, Luisa alikuwa anatapika chakula chote alichokuwa anakila?”“Ndiyo, hali hiyo, lakini, ilikuwa inafahamika na wote, kwa sababu Luisa alipaswa kuishi kwa Utashi wa Mungu peke yake. Lakini watu wengi hawakuamini, na walikuwa wanafikiri kwamba, kitu fulani kilikuwa kinamshibisha.”Jambo hilo nililiona hata mimi, zaidi ya mara moja, nilipokuwa ninakuja kumwona kwao, Luisa.”
- “Na sasa, unataka kufahamu nini zaidi? “Lakini mambo mengi yalikuwa yanaharibika, na katika enzi hizo kama unavyojua, kulikuwa na umaskini mwingi. Hilo mimi pia nililisema kwa Luisa, kwamba hata kama ulaji wake ulikuwa mdogo kiasi gani, karibia kisingemtosha hata mtoto aliyezaliwa wakati huo huo, au saa hiyo hiyo. Na jibu lake lilikuwa ni : “Tunafanya utii.” Hasa, waungamishi juu ya hali hiyo walikuwa na amri maalum kutoka kwa Askofu. Safari moja muungamishi aliniambia kwa sauti kali: “Anapaswa kula siku zote, na wote wanapaswa kuelewa kwamba anakula, vinginevyo, wataweka walinzi mlangoni pake kama walivyofanya kwa Teresa Newmah, pamoja na kelele zote za magazeti.” “Lakini, alikuwa anakunywa maji au vitu vingine vyenye maji maji?” “Mimi sikumpa hata siku moja kinywaji cha maji; alikuwa anakunywa maji ya almondi chungu tu, ambayo dada wa Cimadomo walikuwa wanamletea. Wakati mwingine hata Isa, dada yako, alimtayarishia maji hayo ya almondi, ambayo aliyatoa kutoka kwa shangazi Nunzia. (3) (Nunzia alikuwa dada ya mama yangu, ambaye mumewe alikuwa mkulima).“Je, mandole hayo machungu hayana sumu? Na baada ya muda mrefu, hayaharibu viungo?”
- “Mimi sijui hilo lakini ninaweza kusema kwa hakika, au kwa dhamira safi kwamba, kilikuwa kinywaji pekee alichokuwa anakunywa bila kutapika, au kurudisha kwa mdomo.” “Angalau kilitiwa sukari?” Alinijibu, “hapana- sasa inatosha nimesema karibu karibu kila kitu nilichoweza kusema, na ambacho chote niliweza kufahamu.” “ Lakini mimi ningependa kufahamu zaidi!” “Hapana! Huo ni udadisi tu, kama Luisa atapenda hivyo, nitaweza kukwambia vitu vingine vingi, na sasa, mimi mwenyewe nitakuita.” Hivyo ndivyo nilivyomaliza mazungumzo yangu na shangazi Rosaria. Ilikuwa tarehe 15 Octoba mwaka 1970.
Mfumaji kamili
Licha ya kukatwa sehemu za vidole vya mkono, shangazi Rosalia, kwa mshangao wa watu wote, alikuwa mfumaji kamili wa nakshi, au mapambo ya kutarizi. Alikuwa anakamilisha kazi za Luisa, na akawa mwalimu wa wasichana wote waliokuwa wanafuata kozi ya kutarizi. Zaidi ya hapo alikuwa ni wa lazima sana, na kwa kweli, baada ya kifo cha wazazi wa Luisa alikuwa mtawala wa nyumba yake. Ndiye aliyekuwa anakaribisha au kupokea maagizo au tume mbalimbali, na kukamilisha mikataba au mapatano ya kazi. Lakini hakumwambia mtu yeyote ni zipi zilikuwa nakshi za Luisa, kwa sababu Mutumishi wa Mungu hakupenda kazi yake iwe kitu cha kushangalia, au kuangaliwa kwa namna ya pekee. Baada ya kifo cha Luisa, kazi ya Luisa haikusimama, kwa sababu shangazi Rosaria, alitunza hai mapokeo ya nakshi, iliyostawishwa na Piccarreta au Kadogo (Luisa). Kwamba shangazi Rosaria angekuwa mfumaji kamili, ilionekana kama ni muujiza usio na mwisho. Kwa kila mtu, kwa kuwa ulemavu wake wa mwili, usingemuwezesha kukubali kufanya kazi ambayo ilikuwa ngumu kiasi, au kama hiyo ya kutarizi. Kwa kazi ambazo ziliweza kuwa na thamani ya mamilioni - Kwa kuhitaji miaka mingi ya shughuli, iliombwa kiasi cha kutosha sana au kidogo sana. Kwa sababu hiyo, sisi wapwa wake tulikuwa tunalalamikia shangazi, na yeye alijibu akisema, “Fedha zinapendwa kidogo, jambo la muhimu ni kuweza kuishi.” Shangazi Rosaria alikuwa akitusimulia kwamba, katazo maalum lilikuwa limetolewa na Luisa la kupokea fedha, kwa jina lolote, hasa zawadi au matoleo. Kama, bahati fulani zilifika, kwa njia ya barua, kiasi au fungu la fedha, au kiasi hicho hicho, kilikuwa kinarudishwa kwa yule aliyezituma. Luisa alikuwa anathibitisha kwamba, kwa upande wake, kile alichokuwa nacho tayari, kilikuwa kimezidi na kwamba hakuhitaji kitu chochote.
Fedha hizo kidogo, matunda ya kazi yao, zilikuwa zinatosha kwa mafunzo ya shangazi Rosaria na dada yake Luisa, Angelina. Hilo ni jibu halisi la Mtumishi wa Mungu, alilompa Mwenyeheri Hannibal, alipotaka kumpa haki ya mwandishi, kwa kazi zilizochapishwa akisema: “Mimi sina haki yoyote ile” – Alisema havyo wakati akikataa kupokea fedha aliyokuwa anapewa na mwenyeheri huyo – “ Kwa sababu yale yaliyoandikwa si yangu.”
Majeraha ya Ajabu
Mwaka 1940, kwa shangazi Rosaria, mwanamke au pande la mama, aliyejaa afya, bila ishara yoyote ya maumivu, alianza kuwa na majereha, ambayo kadiri muda ulivyokuwa unapita, yalikuwa yanazidi kuwa makubwa na yenye kuwasha. Kwa namna ya pekee, madonda mawili yalikuwa yanaonekana vizuri sana, yakifanana na majipu makubwa yaliyovimba, yakiwa kabisa chini ya kidevu, Madonda au majeraha haya yalikuwa yanatoa usaa, karibu bila kukoma, na matone mengine yalikuwa yanaanguka kwenye sahani yake, alipokuwa anakula chakula cha mchana. Nilikuwa ninasikia kinyaa kwa hali hii ya kusikitisha, na nikatafuta namna ya kujitenga mbali na meza, lakini mama yangu, ili taabu hiyo isiwe nzito ambayo ililetwa na hali hiyo, alinizuia kwa mkono, wakati mwingine akinifinya sana. Shangazi Rosaria akiwa mmiliki wa pamoja wa mali ya familia, mara moja moja, alikuwa anakuja nyumbani kwetu. Majeraha yake yakiwa yameenea mwilini kote, na hasa kifuani na mabegani, yalikuwa yanatibiwa kwa moyo wa upendo na mama yangu, amb